Mkundi_Housing_Project1

Mradi wa Mkundi

Miliki Nyumba yako leo kupitia Fedha Taslimu au Mkopo wa Nyumba kutoka Benki Washirika. WHC inawajengea Watumishi wa Umma nyumba za bei nafuu katika eneo la Mkundi Morogoro. Uzinduzi wa mradi huu unaonesha Dira thabiti tuliyonayo kwa watumishi wa umma kuweza kumiliki nyumba zao katika maeneo yenye miundominu yakinifu. Wanunuzi wa nyumba hizi wataweza kuishi na kulindwa na “Ibara ya Hatimiliki 2008”, ambayo inazingatia kulinda maslahi ya kila mnunuzi wa nyumba.

Mradi wa Nyumba wa Mkundi ni mradi ambao unatekelezwa katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro umbali wa km 8 kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu na km 0.4 kutoka njia kuu ya Morogoro – Dodoma. Mradi wa Nyumba wa Mkundi unajumuisha nyumba za aina tatu ambazo ni za vyumba viwili zenye ukubwa wa mita za mraba 60 au 61, vyumba vitatu zenye ukubwa wa mita za mraba 85 au 96 pamoja na zile za vyumba vitatu zenye ukubwa wa mita za mraba 115 au 121.
Nyumba ya vyumba viwili inajumuisha vyumba 2 vya kulala, sebule, jiko, bafu, baraza na choo wakati nyumba ya vyumba vitatu inajumuisha vyumba 3 vya kulala (kikiwemo chumba kimoja cha ‘master’) , sebule, jiko, bafu, baraza pamoja na choo.

Faida ya kununua nyumba zetu za Mkundi ni kama ifuatavyo:

  • Ziko umbali wa km 8 tu kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu,
  • Ziko karibu na Shule pamoja Maduka,
  • Uwepo wa vifaa vya michezo kwa watoto,
  • Zipo umbali wa km 0.4 tu kutoka njia kuu ya Morogoro – Dodoma

Bei za Nyumba ni kama zinavyoonekana:

Mkundi_New_Aug2017

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *