kisesa_latest_march2018

Mradi wa Nyumba Kisesa

“Ni bora na rahisi kununua.”

Miliki nyumba yako leo kwa kulipia fedha taslimu au kwa njia ya mkopo kupitia benki washirika.
Watumishi Housing Company inawaletea watumishi wa umma nyumba bora na za bei nafuu katika eneo la Kisesa jijini Mwanza. Uzinduzi wa mradi huu unaonesha dira thabiti tuliyonayo katika kuwawezesha watumishi wa umma kumiliki nyumba katika maeneo yenye miundombinu bora kwa kuishi. Wanunuzi wa nyumba hizi wataweza kuishi kwa kuzingatia (sheria ya hati miliki ya 2008), ambayo inamlinda maslahi ya kila mnunuzi wa nyumba.

Kisesa Mwanza Residence ni Mradi wa Nyumba ambao unatekelezwa katika eneo la Kisesa katika Jiji la Mwanza umbali wa takriban km 20 kutoka Mwanza mjini katika njia kuu iendayo Musoma. Mradi wa Kisesa Mwanza Residence unajumuisha nyumba za aina mbili ambazo ni  nyumba za vyumba viwili na nyumba za vyumba vitatu vya kulala.
Nyumba za vyumba viwili zina ukubwa wa mita za mraba 61 kila moja pamoja na vyumba viwili vya kulala (ikiwemo Master), sebule,jiko,bafu,baraza na choo, ambao nyumba za vyumba vitatu zimegawanyika katika aina mbili kutegemeana na ukubwa wa eneo (mita za mraba 87 na 115). Vyumba vya kulala vya ‘Master’ pia vinapatikana katika nyumba za vyumba vitatu.

Faida kubwa ya kununua nyumba zetu za Kisesa ni kama ifuatavyo:

  • Ziko umbali wa km 20 tu kutoka Mwanza mjini,
  • Ziko karibu na Shule,
  • Karibu na maduka,
  • Uwepo wa vifaa vya michezo kwa watoto.

Bei za Nyumba

kisesa_price

kisesa_price

IMG-20170719-WA0001 IMG-20170719-WA0004 IMG-20170719-WA0005 IMG-20170719-WA0006 IMG-20170719-WA0007 IMG-20170719-WA0008 IMG-20170719-WA0009 IMG-20170719-WA0010 IMG-20170719-WA0011

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *