Njedengwa_latest3

Watumishi Njedengwa Estate

 

Watumishi Njedengwa Estate Dodoma

 

Miliki nyumba yako leo kwa fedha taslimu au kwa njia ya mkopo kutoka Benki washirika.

Watumishi Housing Company inawajengea watumishi wa umma nyumba za bei nafuu katika eneo la Njedengwa katika Manispaa ya Dodoma mjini. Uzinduzi wa mradi huu unaonesha lengo na maono thabiti tuliyonayo katika kuwawezesha watumishi wa umma kuweza kumiliki nyumba katika maeneo yenye miundombinu thabiti na imara. Wanunuzi wa nyumba hizi wataweza kumiliki nyumba hizo kwa kuzingatia sheria ya hakimiliki ya mwaka 2008, ambayo inalinda maslahi ya kila mnunuzi.

Watumishi Njedengwa Estate ni mradi wa ujenzi unaoendelea katika eneo la uwekezaji la Njedengwa lililoko karibu na eneo la Kisasa katika mji wa Dodoma. Awamu ya kwanza ya mradi huu inajumuisha nyumba za aina tatu ambazo ni nyumba ya vyumba vitatu vya kulala yenye ukubwa wa meta za mraba 78 ambayo inajumuisha chumba kimoja chenye Masta, nyumba ya vyumba vitatu vya kulala yenye eneo la meta za mraba 87 ambayo inajumuisha chumba kimoja cha masta pamoja na eneo la makabati na nyumba ya vyumba vitatu vya kulala yenye eneo la meta za mraba 115 ambayo inajumuisha  vyumba viwili vya masta pamoja na eneo la makabati. Aina zote za nyumba zina sebule, jiko, bafu, baraza pamoja na choo.

Bei za nyumba:

 Zingatia kuwa bei ya nyumba ya vyumba vitatu vya kulala iliyokamilika kwa 80% inaanzia shillingi millioni 46.

Aina za Malipo.

  • Mkopo kutoka Benki WashirikaLoan from relevant Bank.
  • Kulipa kidogo kidogo wakati ujenzi ukiendelea kwa makubaliano ya mkataba maalumu.
Mchoro - Mradi wa Njedengwa Dodoma
Mchoro – Mradi wa Njedengwa Dodoma
Mchoro - Mradi wa Njedengwa Dodoma
Mchoro – Mradi wa Njedengwa Dodoma
Nyumba ya vyumba vitatu vya kulala (meta za mraba 115)
Nyumba ya vyumba vitatu vya kulala (meta za mraba 115)
Site Plan - Njedengwa Dodoma Estate
Site Plan – Njedengwa Dodoma Estate
Nyumba ya vyumba vitatu vya kulala (meta za mraba 87)
Nyumba ya vyumba vitatu vya kulala (meta za mraba 87)

 

Nyumba ya vyumba vitatu vya kulala (meta za mraba 78)
Nyumba ya vyumba vitatu vya kulala (meta za mraba 78)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *