Magomeni_new_new2

Watumishi Magomeni Apartments

“Ni bora na bei nafuu.”

Miliki nyumba yako leo kwa pesa taslimi au kwa mkopo wa nyumba utoka benki washirika. Watumshi Housing Company inawaletea watumishiwa umma nyumba za bei nafuu zilizopo eneo zuti lililo katiati ya mji maeneo ya magomeni. Uzinduzi wa mradi huu unaonyesha dira nzri ambayo inawawezesha watumishi wa umma kupata na kuishi kwenye makazi yaliyo bora na ya kisasa. Wanunuzi wa nyumba hizi wataishi kwenye nyumba zao kwa kuzingatia mfumo wa hati pacha (Unit titles Act 2008). Wale watakao nunua nyumba kwa mfumo huu wataishi kwa kuzingatia sheria hii ambayo imeundwa kulinda maslahi ya kila mnunuzi.

Watumishi Magomeni Appartments ni mradi wa nyumba ambazo zipo kwenye majengo mawili yenye ghorofa 15 na mradi huu upo karibu na kituo cha polisi cha usalama magomeni. Ghorofa mbili zilizoenda chini ni kwa ajili ya maegesho ya magari,ghorofa ya kwanza ni sehemu ya maduka, ofisi pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii. Watumishi Magomeni Appartments ina nyumba za aina mbili.Nyumba za vyumba viwili na vyumba vitatu.Nyumba ya vyumba viwili yenye ukubwa wa mita za mraba 60 ina vyumba viwili vya kulala,sebule,jiko,laundry,veranda na choo. Nyumba ya vyumba vitatu ni kama nyumba ya vyumba viwili ila hii ina vyumba vya kulala vitatu.

Sifa Nyingine za nyumba hizi ni kama ifuatavyo:

  • ┬áZipo pembezonimwa barabara ya morogoro road.
  • Zipo karibu na shule.
  • Zina sehemu ya maduka na sehemu za kuegeshea magari.
  • ┬áZipo katikati ya mji.

magomeni-gharama

Njia za malipo.

  • Mkopo kutoka benki husika.
  • Kulipa kidogo kidogo wakati wa ujenzi wa mradi ukiwa unaendelea kwa makubaliano maalum.