Nyumba na Makazi

WHC inauza aina tofauti za nyumba zinazokidhi mahitaji ya mteja. Kwa kutegemeana na mahitaji ya mteja, nyumba zinazouzwa ziko kuanzia za vyumba 2 vya kulala hadi vyumba 4. Nyumba za WHC pamoja na makazi zinajengwa kwa kuzingatia utamaduni halisi wa Mtanzania pamoja na maisha ya vijana wa kisasa. WHC ilifanya utafiti wa aina za nyumba zinazohitajika, hivyo michoro ya usanifu majengo wa nyumba hizi umezingatia maoni na matakwa ya wateja wetu. Inapotokea kuna sababu maalumu, mteja anaweza akaomba kufanyike maboresho au marekebisho katika michoro ya usanifu kwa nyumba aliyoichagua.

Huduma za uwekezaji

WHC ni msimamizi wa dhamana ya uwekezaji katika ardhi na nyumba ambaye kimsingi anasimamia fedha za ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa umma kwa njia ya shughuli za uwekezaji katika vipande (REITS). Kwasasa, vipande vyote vinamilikiwa na wanahisa wa WHC na hivyo kwa sasa hakuna mauzo ya vipande katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hata hivyo, baada ya kipindi hiki cha miaka mitatu vipande vitaweza kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, ambapo Wananchi watapata fursa ya kuwekeza katika kuuza au kununua vipande vya WHC-REIT

Usimamizi wa Miliki

WHC pia ina jukumu la kutoa huduma za usimamizi wa miliki kwa majengo ya makazi na biashara. Pale zitakapoanza, kazi hiyo itafanywa na timu ya wataalamu wanaolijua vema soko la Tanzania. Katika usimamizi wa miliki, huduma nyingine zitakazotolewa ni pamoja na:

  1. Upangishaji wa majumba.
  2. Uendeshaji hoteli.
  3. Mipango miji.
  4. Uwakala (estate agency).
  5. Upimaji na thamani za viwanja.

Upimaji na Uendelezaji Miundombinu ya Viwanja

Kupitia shughuli za ubia, WHC inafanya kazi na halmashauri ya miji na manispaa kupima viwanja kwa ajili ya makazi, biashara na kanda maalumu za kiuchumi (EPZ). Aidha, WHC inaweza kufanya uwekezaji kwa ubia na manispaa au