Wafuatao wana vigezo vya kununua nyumba za WHC:
- Wafanyakazi wanaofanya kazi katika serikali kuu, serikali za mitaa, mashirika ya umma, idara binafsi au taasisi nyingine za umma;
- Wafanyakazi wanaofanya kazi katika sekta binafsi au wajasiriamali walioajiriwa ambao ni wanachama wa Mifuko ya Pensheni kwa hiari au kisheria;
- Wanachama wa Mifuko ya Pensheni;
- Watanzania wanaofanya kazi katika Mashirika ya Kimataifa ambayo Tanzania inahusishwa;
- Watanzania wanaoishi nje ya nchi ambao ni wanachama wa mifuko ya pensheni (kisheria au kwa hiari); pamoja na
- Watumishi wa umma waliostaafu.