Skip to main content
HATUA NANE (8) RAHISI ZA KUMILIKI NYUMBA YAKO:
- Chukua fomu yya kununua nyumba toka ofisi ya WHC au kwenye tovuti ya WHC.
- Rudisha fomu iliyojazwa ikiwa na uthibitisho kuwa ni mwajiriwa wa serikali,wakala wa serikali za mitaa idara zinazojitegemea,mashirika ya umma,sahihi ya mwajiri au kiongozi wa taasisi unapofanyia kazi.
- Ada ya maombi ni sh 10,000.
- Maombi yako yatapitiwa kwa umakini kulingana navigezo na masharti ya WHC.
- Kama umefanikiwa utataarifiwa kwa barua kuthibitisha kukubaliwa maomi yako. Barua zitatolewa kwa wote waliokidhi vigezo vilivyotolewa.
- Mauzi ya nyumba za mradi husika yatatangazwa kuwa yamefungwa pindi idadi ya waombaji imefika idadi ya nyumba zilizopo kweye mradi huo.
- Unaweza kulipia nyumba kupitia njia zifuatazo:
- Kulipia kidogo kidogo wakati shughuli za ujenzi mradi wa nyumba zikiwa zinaendelea na kisha kumalizia kiasi kilichobaki wakati mradi unapokamilika.
- Kwa kutumia njia ya mkopo wa muda mrefu ‘Mortgage’ na benki husika.
- Kutumia njia ya mkopo maalum (‘Tenant purchase’). Mfano: Mradi wa Mkundi.
- Kulipa taslimu (Ununuzi wa moja kwa moja).
- WHC itafanya utaratibu wa kutafuta hati za nyumba na kisha kuwapatia wanunuzi walioweza kulipa pesa.