MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

  1. Wafanyakazi wanaofanya kazi katika serikali kuu, serikali za mitaa, mashirika ya umma, idara binafsi au taasisi nyingine za umma;
  2. Wafanyakazi wanaofanya kazi katika sekta binafsi au wajasiriamali walioajiriwa ambao ni wanachama wa Mifuko ya Pensheni kwa  hiari  au kisheria;
  3. Wanachama wa Mifuko ya Pensheni;
  4. Watanzania wanaofanya kazi katika Mashirika ya Kimataifa ambayo Tanzania inahusishwa;
  5. Watanzania wanaoishi nje ya nchi ambao ni wanachama wa mifuko ya pensheni (kisheria au kwa hiari); pamoja na
  6. Watumishi wa umma waliostaafu.

Ndio inawezekana, nyumba zinategemewa kuuzwa kwa bei tofauti tofauti. Wafanyakazi wa WHC pamoja na benki washirika watakupa ushauri fasaha juu ya nyumba sahihi unayopaswa kuomba kununua.
Ndio kuna faida nyingi sana kununua nyumba kutoka WHC. Kwanza, ni kwamba nyumba hizi zinategemewa kuwa na ubora wa hali ya juu kwa maana zimedhaminiwa na Serikali pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Pili, Utaweza kuhamia kwenye nyumba hizi pindi tu ujenzi utakapomalizika tofauti na utakapoamua kujenga nyumba yako mwenyewe ambapo huchukua muda kuhamia. Tatu, utapata hati miliki ya nyumba yako bila usumbufu na nne kwa kuwa na nyumba za WHC, unahakikishiwa kuwa na ujirani mwema.
Hakuna uhitaji wowote wa kulipa fedha kama kianzio. Hata hivyo, waombaji wanashauriwa kuhakikisha wanakuwa na kiasi fulani cha fedha ili kupunguza makali ya mkopo wakati wanapotaka kununua nyumba. Hii itamsaidia mteja kulipa kiasi kidogo kwa mwezi wakati wa kurudisha mkopo.
WHC inajenga nyumba za aina mbalimbali yaani moja moja zinazojitegemea, nyumba mbili zinazotegemeana pamoja na nyumba za magorofani. Hata hivyo nyumba za magorofani zimesanifiwa kwa kuzingatia kanuni za kisasa kabisa kuweza kukabiliana na mahitaji ya mteja.
Mkopo wako wa nyumba utakuwa na bima pamoja na dhamana iliyowekwa na Mfuko wako wa Hifadhi ya jamii. Hii itakuhakikishia kuwa ikitokea bahati mbaya ukafariki kabla ya kumaliza mkopo, warithi wako hawatanyang’anywa nyumba.
Ili kupata ushauri yakinifu, wasiliana na WHC au benki washirika ili kuweza kupatiwa ushauri juu ya kipato chako na kiwango cha mkopo unachoweza kulipa ili kuweza kununua nyumba ya WHC.
Hapana, wageni hawaruhusiwi kununua nyumba za WHC..
Unaweza kupiga simu moja kwa moja Ofisi za WHC kupitia (+255 22 2922211) au andika barua pepe kisha tuma kwenda info@whc.go.tz au andika barua kupitia S.L.P 5119 DSM. Pia unaweza kutembelea moja kwa moja katika Ofisi za NHC zilizopo katika kila mkoa wa Tanzania Bara au unaweza kupiga simu moja kwa moja kwa Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mwasiliano (0716 290 355) au Mkurugenzi wa Uendeshaji (COO) Mkurugenzi Mtendaji  +255 754 304 833..
Mkopo unaweza kurudishwa kuanzia kipindi cha mwaka mmoja hadi miaka 25 kutegemeana na uwezo wa mteja kifedha. WHC itasaidia katika zoezi la kufanikisha wateja wote wanaotaka kumaliza kurudisha mikopo yao mapema kama wanaweza kufanya hivyo.
Mkopo wako wa nyumba utafidiwa na Mwajiri wako pamoja na mafao yako kutoka Mfuko wa Hifadhi ya jamii. Kama ikitokea kwa bahati mbaya umefariki kabla ya kumaliza kulipa mkopo wako wa nyumba, mafao yako yatatumika kufidia kiasi cha mkopo kilichobaki.
YesNdio, pindi tu utakapokuwa umechagua nyumba unayoihitaji na mradi husika ukiwa tayari umeshaanza, unaweza kuanza kulipia nyumba yako. Utaweza kukabidhiwa nyumba yako punde tu shughuli za ujenzi zitakapokamilika..