Kuhusu Watumising Housing Company:

WHC-REIT inamilikiwa na Taasisi nne zikiwamo Taasisi mbili za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (yaani: PSSSF na NSSF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Shughuli kubwa za WHC-REIT kwa ujumla ni:

  1. Utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma (PSHS)
  2. Kusimamia dhamana ya uwekezaji katika ardhi na nyumba.
  3. Kujenga, kukarabati au kuboresha majengo kwa ajili ya kupangisha au kwa shughuli nyingine za kiuchumi.
  4. Kujishughulisha na biashara ya usimamizi wa miliki.
  5. Kufanya makubaliano ya kuingia ubia au ushirikiano na Kampuni yoyote au mtu yeyote ambaye anashughulika na biashara ambazo zinaendana na malengo ya WHC.

WHC inaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi ambayo inajumuisha Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi zote zinazoimiliki. Pia katika Bodi hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawakilishwa na wajumbe walioteuliwa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Ofisi ya Rais – Utumishi wa umma. Shughuli za kila siku za WHC zinasimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji (CEO) akisaidiana na Mkurugenzi wa Uendeshaji (COO) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha  na Utawala (CFO). WHC inazingatia kuendelea kuwa na ubora katika utendaji kazi ambao unazingatia malengo yake.

Dira: Makazi bora kwa watumishi wa umma.

DhimaKuwasaidia watumishi wa umma kuweza kumiliki nyumba kupitia mikopo ya bei nafuu pamoja na kujishughulisha na biashara zenye faida katika uwekezaji wa miliki kwa kuzingatia kanuni bora za usimamizi wa fedha.