Miradi ya Ujenzi:

WHC imeanza kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba. Miradi hiyo inatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2014/2015. Wakati ambapo miradi ifuatayo imepangwa kukamilika katika awamu ya kwanza ya utekelezaji, zoezi la kutwaa ardhi katika maeneo mengine bado linaendelea ambapo miradi mingine zaidi inategemea kutekelezwa katika awamu nyingine.


MAHALI MRADI UFAFANUZI WA MRADI
Pwani Kibaha-Mailimoja Setelite City Magorofa 100 yatajengwa pembezoni mwa barabara kuu ya Morogoro katika eneo la Kibaha Mailimoja.
Dodoma Njedengwa Housing Project (Udom Road) Nyumba 100 za aina tofauti zitajengwa katika eneo la uwekezaji  mjini Dodoma ambapo tayari kuna barabara nzuri, maji na huduma za umeme.
Morogoro Mizani Mkundi Housing Project (Dodoma Road) Nyumba 47 zitajengwa katika eneo ambalo liko umbali wa mita 100 kutoka barabara kuu ya Dodoma na km 10 kutoka eneo la Msamvu.
Mtwara Mangamba Housing Project (Airport Road) Eneo lililoendelezwa lililopo pembezoni mwa barabara iendayo Uwanja wa ndege.
Mbeya Tunduma-Mpemba Housing Project Mradi wa ujenzi wa nyumba za vyumba 2 hadi 3 katika eneo la mji wa Tunduma.
Tanga Pongwe City Housing Project Eneo lililopo m 100 kutoka pembezoni mwa barabara na km 18 kutoka Tanga mjini.
Mwanza Kisesa Housing Project Mchanganyiko wa nyumba za kawaida pamoja na ghorofa katika eneo lililopimwa la Kisesa Mwanza.
Shinyanga Shinyanga Housing Project  
Arusha USA River Housing Project Eneo la makazi lenye kijani kibichi lililoko km1.5 kutoka barabara kuu iendayo Arusha katika eneo la mji wa USA River karibu na Hoteli ya Ngurdoto.
Lindi Mtwelo Beach Housing Project Mradi uliopo eneo la Mtwelo Beach katika eneo lililopimwa katika mji wa Lindi
Dar-Es-salaam

  • Bunju- Mabwepande Housing Project
  • Kigamboni-Gezaulole Housing Project
  • Watumishi Magomeni Flats

Mchanganyiko wa nyumba za kawaida kati ya vyumba 2 hadi 3. Pia kutakuwa na ghorofa na nyumba nyingine za kawaida.