Kuna njia 4 tofauti ambazo unaweza kuzitumia kulipia nyumba:


  • 1.0 Kulipia kidogo kidogo wakati ujenzi wa mradi wa nyumba husika ukiendelea, na wakati mradi unapokamilika, unaweza kuchukua mkopo kutoka benki au SACCOS au kutoka mfuko wako wa Hifadhi ya Jamii kumalizia kiasi kilichobaki. Mkopo huo unaweza kurudishwa kidogo kidogo kila mwezi haid kufikia miaka 25.
  • 2.0 Kulipia kwa kutumia mkopo wa nyumba ‘mortgage’ kupitia benki husika au benki yeyote utakavyochagua. WHC imeingia mikataba ya makubaliano na benki za CRDB, AZANIA, EXIM, BOA na NMB katika kutoa mikopo ya gharama nafuu kwa Watumishi wa Umma.
  • 3.0 Kwa baadhi ya miradi mfano Mradi wa ‘Mkundi-Morogoro Residence’ unaweza kununua nyumba yako moja kwa moja kupitia WHC kwa njia ya Mpangaji Mnunuzi¬†ambapo baada ya kulipia 5% ya bei ya nyumba kama kianzio, utaweza kurudisha mkopo wako kwa kipindi cha kuanzia mwaka mmoja hadi miaka 25 kutegemeana na uwezo wako.
  • 4.0 Unaweza kulipa taslimu.